The Madonna of the Streets
Mary's Rosaries

Home Page

Contact Us

Make a Payment, Methods of Payment, Refund and Exchange Policies

Rosaries
subpages:

How to Pray the Rosary
subpages:

Pictures Main Page
subpages:

Curriculum
subpages:

Website Terms of Use

License Agreement

Sitemap


The Work of God's Children

 Swahili Rosary Prayers
 
Swahili is also known as Kisweheli, Suahili, Kisuahili, and Arab-Swahili.
This language is spoken by 541,000 people in Tanzania and by 131,000 people in Kenya.  This is the most widespread language in eastern Africa.  It is also spoken in the eastern parts of the Democratic Republic of the Congo.

See also The Work of God's Children page for the illustrated version of prayers in this language.

Ishara Ya Msalaba / Sign of the Cross / Signum Crucis
 Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina!


Imani Ya Mitume / The Apostles' Creed
  Ninamwamini Mungu, Baba Mwenyezi,
Muumba wa mbingu na dunia;
 
Na Yesu Kristo,
Mwana wake wa pekee, Bwana wetu,
aliyetwaa mwili kwa tendo la Roho Mutakatifu,
akazaliwa na Bikira Maria.
Akateswa zamani za Pontio Pilato,
akasulibiwa, akafa, akazikwa,
akashuka kuzimuni mwa wafu,
akafufuka katika wafu siku ya tatu,
akapanda mbinguni,
anakaa kwa mukono wa kuume wa Mungu,
Baba Mwenyezi,
ndipo atakuja tena kuhukumu wazima na wafu.
 
Ninamwamini Roho Mutakatifu,
Kanisa katolika takatifu,
ushirika wa watakatifu,
ondoleo la zambi,
ufufuko wa mwili,

     na uzima wa milele. 
     Amina.

UAMINIFU WA WAFUATA / The Apostles' Creed / Credo

Nina amini Mungu Baba Nguvu Zote, Muuabaji wa Bingu na Dunia; na Yesu Kristo, Mwana pekee wa Mungu, Mwokozi wetu; ambaye aliumbwa

na Roho Mtakatifu, na kuzaliwa na bikira Maria, akateswa na Pontias Pilato, akasurubiwa msalabani, akafa na akazikwa; akaenda kwa shetani; na siku ya

tatu akafufuka kaburini; alienda binguni, na hukaa katika Mkono wa kulia wa Mungu Baba wa Binguni; kutoka huko atakuja kuwahukumu wanaoishi na waliokufa. Nina amini katika Roho Mtakatifu; nina amini katika

utakatifu wa kanisa ya katolika; na kushiriki kwa watakatifu; kusamehewa kwa dhambi; kufufuka kwa mwili; na maisha milele, Amina.

Baba Yetu / Our Father / Pater Noster
Baba yetu, uliye mbinguni Jina lako litukuzwe, ufalme wako ufike, utakalo lifanyike duniani kama mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kila siku, utusamehe makosa yetu, kama nasi tunavyowasamehe waliotukosea. Usitutie kishawishini bali utuopoe maovuni. Amina.

 

Another version of

Baba Yetu / Our Father
Baba yetu uliye mbinguni,
jina lako litukuzwe.
Ufalme wako ufike.
Utakalo lifanyike duniani mbinguni.
Utupe leo mkate wetu wa kila siku.
Utusamehe makosa yetu,
kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea.
Usitutie katika kishawishi,
lakini utuopoe maovuni.
Amina.

Another version of

Baba Yetu / Our Father
Baba yetu uliye mbinguni,
jina lako litukuzwe.
Ufalme wako ufike.
Utakalo lifanyike duniani mbinguni.
Utupe leo mkate wetu wa kila siku.
Utusamehe makosa yetu,
kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea.
Usitutie katika kishawishi,
lakini utuopoe maovuni.
Amina.

Another version of

Baba Yetu / Our Father 
Baba yetu uliye mbinguni,
jina lako litukuzwe.
Ufalme wako ufike.
Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.
Utupe leo mkate wetu wa kila siku.
Utusamehe makosa yetu,
kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea.
Usitutie katika kishawishi,
lakini utuopoe maovuni.
Amina.

Another version of

Baba Yetu / Our Father
Baba yetu uliye mbinguni
Jina lako litukuzwe
Ufalme wako ufike
Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni
Utupe leo mkate wetu wa kila siku
Utusamehe makosa yetu
kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea
Usitutie katika kishawishi
lakini utuokoe maovuni.
Amina.

Another version of
Baba Yetu / Our Father
Baba yetu uliye mbinguni: Jina lako litukuzwe. Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni. Utupe leo chakula chetu tunachohitaji. Utusamehe makosa yetu, kama nasi tunavyowasamehe waliotukosea. Usitutie katika majaribu, lakini utuokoe na yule Mwovu. Amen.

Another version of

Baba yetu / Our Father / Pater Noster
Baba yetu uliye mbinguni,
Jina lako litukuzwe,
Ufalme wako uje,
Mapenzi yako yatimizwe,
hapa duniani kama huko mbinguni.
Utupe leo riziki yetu.
Utusamehe deni zetu,
kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.

Na usitutie majaribuni,
lakini utuokoe na yule mwovu.

Amina.

Doxology
Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele.


This is the pronunciation key for
Baba Yetu / Our Father / The Lord's Prayer
in Swahili:
English: Our Father Who Art In Heaven
Swahili: BABA YETU ULIYE MBINGUNI
Phonetics: Bah-Bah Yay-too You-lee-yay mm-been-goo-nee
English: Hallowed Be Thy Name
Swahili: JINA LAKO LITU KUZWE
Phonetics: Gee-Nah La-co Lee-too Kooz-way
English: Thy Kingdom Come
Swahili: UFALME WAKO UJE
Phonetics: You-Fahl-may Wah-co You-jay
English: Thy Will Be Done
Swahili: MAPENZI YAKO YATIMIZWE
Phonetics: Mah-pain-zee Yah-co Yah-tee-meez-way
English: On Earth as it is in Heaven
Swahili: HAPA DUNIANI KAMAHUKO MBINIGUNI
Phonetics: Hap-pah Do-nee-ah-nee Kah-mah-who-co M-been-goo-nee
English: Give Us This Day
Swahili: UTUPE LEO RIZIKI YETU
Phonetics: Yoo-too-pay Lee-oh Ree-zee-kee Yay-too
English: Our Daily Bread
Swahili: UTUSAMEHE DENI ZETU
Phonetics: You-too-sah-may-hay Day-nee Zay-too
English: And Forgive Us Our Debts As We Forgive Our Debtors
Swahili: KAMA SISI NASI TUWASAMEHEVYO WADENI YETU
Phonetics: Kah-mah see-see Nah-see (Too-wah-sah-may-hayv-yoh) wah-day-nee ya-too
English: Lead Us Not Into Temptation
Swahili: NA USITUTIE MAJARABUNI
Phonetics: Nah you-see-too-tee-a Mah-jah-rah-bu-nee
English: But Deliver Us From Evil
Swahili: LAKINI UTUOKOE NA YULE MWOVU
Phonetics: Lah-kee-nee You-too-oh-coay Nah-you-lay Mwo-voo
English: Amen
Swahili: AMINA
Phonetics: Ah-Mee-Nah

Salam Maria / Hail Mary / Ave Maria
Salam Maria, umejaa neema, Bwana yu nawe, umebarikiwa kuliko wanawake wote na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria mtakatifu mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.


Another version of
Salamu Maria / Hail Mary
Salamu, Maria, umejaa neema,
Bwana yu nawe,
umebarikiwa kuliko wanawake wote,
na Yesu, mzao wa tumbo lako amebarikiwa.
Maria mtakatifu, Mama wa Mungu,
utuombee sisi wakosefu,
sasa na saa ya kufa kwetu.
Amina.

Another version of
Nakwamkia Maria / Hail Mary
Nakwamkia Maria,
umejaa nema, Rabbi yu
kwako; una baraka wewe
kuliko wanawake na
Yesu mzao wa tumbo
lako ana baraka.
Maria mtakatifu, mama
wa Mungu, utuombee sisi
wakosefu, sasa na saa ya
kufa kwetu.
Amina.

Another version of
Salamu Maria / Hail Mary
Salamu Maria,
umejaa nema,
Bwana yu nawe,
Umebarikiwa kuliko wanawake wote,
Na Yesu msao kwa tumbo lako amebarikiwa,
Maria mtakatifu mama wa Mungu,
Utuombee sisi wakosefu,
sasa na saa ya kufa kwetu.
Amina.

Another version of
Nukuamkia Maria / Hail Mary
Nukuamkia Maria, umejaliwa neema,
Bwana ni nawe,mbarikiwa wee
kuliko wanawake wote,na mbarikiwa mtote wa tumbo lako Yesu.
Maria mtakatifu,Mama wa Mungu,utuombee sisi wakosefu,
sasa na wataki wa kufa kwetu.
Amina.

Another version of
Nakusalimu (nakuamkiya) Maria / Hail Mary / Ave Maria
Nakusalimu (nakuamkiya) Maria
umejaliwa neema,
Bwana ninawe. Mubarikiwa wewe kuliko wanawake wote,
na mubarikiwa mtoto wa tumbo lako Yesu.

Maria mtakatifu, Mama wa Mungu,
utuombeye sisi wakosefu,
sasa na wakati wa kufa kwetu.

Amina.

Another version of
Salam Maria / Hail Mary / Ave Maria
Salam Maria umejaa neema Bwana yu nawe umebarikiwa kuliko wanawake wote na Yesu mzao wa tumbo lako amabaliki wa.
Maria Mtakatifu mama wa Mungu utuombee sisi wakosefu sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.


Atukuzwe Baba / Glory Be
Atukuzwe Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu.
Amina.

Atukuzwe Baba / Glory Be
Atukuzwe Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu.
Kama mwanzo, na sasa, na siku zote, na milele.
Amina.


Ee Yesu wangu / Oh, My Jesus (Fatima Prayer)
Ee Yesu wangu, utusamee dhambi zetu, utukinge na moto wa milele, ongoza roho zote Mbinguni hasa za wale wanao hitaji zaidi Huruma yako.

SALAM, MALKIA! / Hail, Holy Queen / Salve Regina

Salam, Malkia! Mama mwenye huruma uzima tulizo matumaini yetu. Salam! Tunakusihi ugenini sisi wana wa Eva. Tunakulilia tukilalamika na kuhuzunika huku bondeni kwenye machozi. Haya basi mwombezi wetu utuangalie kwa macho yako ya huruma, Na mwisho wa ugeni huu utuonyeshe Yesu mzao mbarikiwa wa tumbo lako. Ee mpole, Ee mwema, Ee mpendelevu Bikira Maria.

NAMNA YA KUISALI / How to Pray the Rosary

* Baada ya ishara ya msalaba, tunasali Atukuzwe Baba na zile sala pili za utangulizi, halafu tunalitangaza fumbo; inafuatiwa na Baba yetu (1),Salamu Maria (10) halafu Atukuzwe Baba… na zile sala pili za utangulizi.
Halafu tunatangaza fumbo linalofuata na kuendelea kama ilivyoelezwa hapo juu.
* kwa namna ya pekee wakati wa kusali “Baba yetu” na “Salamu Maria” (10) fanya akili (na moyo!) “kukimbilia” kutafakari juu ya fumbo lililotangazwa.


Ishara Ya Msalaba / Sign of the Cross
+ Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina!

Atukuzwe Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, kama mwanzo na sasa na siku zote na milele. Amina.
Kubarikiwe siku zote kutungwa mimba bila dhambi ya asili kwa Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu na Mama yetu.
Ee Yesu wangu, utusamee dhambi zetu, utukinge na moto wa milele, ongoza roho zote Mbinguni hasa za wale wanao hitaji zaidi Huruma yako.

(Tunatangaza Fumbo)

Baba yetu, uliye mbinguni Jina lako litukuzwe, ufalme wako ufike, utakalo lifanyike duniani kama mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kila siku, utusamehe makosa yetu, kama nasi tunavyowasamehe waliotukosea. Usitutie kishawishini bali utuopoe maovuni. Amina.
Salam Maria, umejaa neema, Bwana yu nawe, umebarikiwa kuliko wanawake wote na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria mtakatifu mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu sasa na saa ya kufa kwetu. Amina. (mara 10).MAFUMBO YA UUMBAJI

( kwa Jumatatu) :

 1. YHWH: Mungu Baba kwa njia ya Neno (ΛΟΓΟΣ – VERBUM), [“Awe!”], aumba mbingu na dunia na Roho Mtakatifu ambaye tayari aliutangulia uumbaji kwa hekima yake alikuwa akielea juu ya maji yaliyo kuwa yameufunika uso wote wa nchi akivibariki viumbe.

 2. Mungu amuumba mtu, mwanamme na mwanamke, wote aliwaumba kwa mfano na sura yake.

 3. Mungu amwahidia mwanmke baada ya dhambi ya asili kuwa kwa njia ya uzao wake, Masiha ataponda kichwa cha nyoka – adui wa mwanadamu.

 4. Melkisedeki kuhani mkuu atoa mkate na divai kama sadaka ya shukrani kwa ushindi wa babu mtakatifu Abrahamo (Mwa. 14, 18-20).

 5. Abrahamo aupokea ugeni, atambua na “kumkaribisha” Bwana, Utatu Mtakatifu karibu na mialoni ya Mamre (Mwa. 18, 1-15).

 6. Mungu amweka huru Isaka toka mauti kulingana na ahadi yake(“uzao wako utakuwa mwingi kuliko nyota za mbinguni na kuliko mchanga ulioko pwani ya bahari na kuimiliki miji ya adui zako” – (Mwa. 22, 17) na kuimarisha Agano lake na Abrahamo (“na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia(Mwa. 22, 18).

 

MAFUMBO YA NGUVU ZA MUNGU

( kwa Jumane) :

 1. MUNGU, katika nafsi yake, awaokoa watu wake toka utumwani Misri na kuizindua Pasaka ya kwanza ya “umilele” (Kut. 12, 1-15).

 2. MUSA – mfano wa KRISTO - kwa Bakora aigawanya bahari ya Sham kwa ajili ya njia na uzima wa taifa teule na kuwaangamiza maadui wa Israeli kama isemavyo zaburi ya pili(Zab. 2, 8-9) ya mfalme masiha “uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako, na miisho ya dunia kuwa milki yako. Utawaponda kwa fimbo ya chuma, na kuwavunja kama chombo cha mfinyanzi.” na kama kisemavyo kitabu cha ufunuo wa Yohana (Ufu. 12, 5) “naye atamzaa mtoto wa kiume atakaye yatawala mataifa yote kwa fimbo ya chuma na mtoto alichukuliwa mara moja mbele ya Mungu na mbele ya kiti chake cha enzi”.

 3. NGUVU YA MUNGU, katika namna ya wingu ikatulia juu ya sanduku la agano Ambalo lilikuwa limewekwa katikati ya kambi ya wana wa Israeli ambalo katikati Yake kuna tabernakulo takatifu ambamo ndani yake Mungu ana kaa na ambamo taifa teule litapewaishara tatu zilizokielezo cha Ekaristia Takatifu na Tabernakulo ya Ekaristia Takatifu:Vibao vya Sheria, yaani Neno lake (Verbum), “lililoandikwa kwa kidole cha Mungu” (hivyo kuja kwake moja kwa moja kama Mwana); Bakora ya Musa ni ishara nguvu aliyopewa na Mungu ambayo kwayo Musa aliigawanya ya Sham; Manna iliyoshuka toka mbinguni na ambayo huwashibisha wana wa Israeli huko jangwani.

 4. MUNGU amchagua Daudi na kumpaka mafuta kama Mfalme na Nabii juu ya watu wake Israeli na kuahidi Ufalme Milele kwa mwanae (katika uzao wake).

 5. JUDITA Jd. 8-16), anayekata kichwa cha mfalme, adui wa wana wateule akiwaweka huru toka utumwani ni mfano wa MARIA aliyevaa jua na mwezi chini ya miguu yake na taji la nyota kumi na mbili ambayo huseta kichwa cha mfalme wa giza, “nyoka wa kale”, na kuwaweka huru wateule wa Kristo toka utumwa wa yule mwovu.

 6. NGUVU YA ROHO MTAKATIFU inajionyeshe pia Katika ushahidi wa mzee Eleazaro (2 Mak. 6, 18-31), katika watakatifu ndugu wa Makabayo na Mama yao Mtakatifu (2 Mak. 7, 1-41), kwa kutokukubali kuiasi Sheria ya Mungu.

 

MAFUMBO YA FURAHA / The Joyful Mysteries

( kwa Jumatano) :

 1. Malaika mkuu Gabrieli ampasha habari Bikira Maria, na kwa “NDIYO” Yake, NAFSI YA PILI YA UTATU MTAKATIFU INAJIMWILISHA KATIKA TUMBO LAKE.

 2. Maria Mtakatifu amtembelea Mtakatifu Elizabeti.

 3. YESU ANAZALIEWA BETLEHEM.

 4. Yesu anatolewa Hekaluni ili aweze kutolewa sadaka kwa mungii Baba.

 5. Yesu anakutwa Hekaluni.

 

MAFUMBO YA MWANGA / The Luminous Mysteries

( kwa Alhamisi) :

 1. Yesu anabatizwa katika mto Jordan na Yohana Mbatizaji.– (Yesu anajipeleka kwa Yohana Mbatizaji ili aweze kubatizwa naye. Yeye habatizwi kwa ajili ya toba bali anapenda “kujishusha” zaidi na kujifanya mdhambi (ila bila dhambi) kati ya wadhambi. Mara baada ya kuingia majini mbingu zinafunguka, Roho Mtakatifu katika umbo la njiwa anatua juu yake na sauti ya Baba inatangaza toka juu mbinguni “Huyu ni Mwanangu mpendwa wangu niliyenipendezwa naye” - Mt. 3, 17).

 2. Yesu anafanya ishara ya kwanza katika maisha yake hadharani katika harusi ya Kana. -(Yesu alikuwa amealikwa pamoja na wanafunzi wake katika harusi ya Kana ya Galilaya. Wakiwa wameishiwa divai Yesu analetewa ombi na mama yake, anabadili maji kuwa divai. Injili inayoeleza tukio hilo inataarifu maneno ya mwisho ya mama Maria akituonya na kutualika daima kwamba «LOLOTE ATAKALOWAAMBIA, FANYENI !» - Yn. 2, 5).

 3. Yesu atangaza ujio wa ufalme wa Mungu. -(Yesu anatangaza kuwa ufalme wa Mbinguni u karibu na kwamba uko tayari kati yetu na kuthibitisha kuwa wataingia humo wale tu walioisafisha mioyo yao na kujinyenyekesha hata kujifanya «wadogo» kama mtoto).

 4. Yesu anabadilika sura katika utukufu wa Mungu juu ya mlima Tabor pamoja na Musa na Elia. - (Yesu anapanda mlima Tabor akiwa pamoja na Pietro, Yakobo na Yohana ili kusali. Mara kwa ghafla anabadilika sura katika utukufu wake wa kimungu anangara kuliko jua, karibu naye wanatokea Musa na Elia wakijadiliana kuhusu utume wake wa kimasiha kwa ajili ya wokovu, kwao yampasa aikabili Yerusalemu. Baba anatualika na anamtolea tena ushuhuda “Huyu ni Mwanangu mpendwa wangu ninayependezwa naye:MSIKILIZENI YEYE” - Lk. 9, 35).

 5. Yesu akiwa anaadhimisha Pasaka ya Kiebrania pamoja na Mitume wake katika ukumbi wa mlo wa jioni aliweka Ekaristia Takatifu. - (Juu ya mlima Sion, katika ukumbi wa Chakula cha Jioni, Yesu, akiwa anaadhimisha Pasaka ya Kiebrania pa moja na Mitume wake baada ya kuwa amewaosha miguu aliwapa mkate na divai akithibitisha ni mwili wake na damu yake vilivyotolewa kwa ajili ya wokovu wa watu wote. Ni adhimisho la Ekaristia Takatifu).

 

MAFUMBO YA UCHUNGU / The Sorrowful Mysteries

( kwa Ijumaa) :

 1. Yesu asali katika bustani ya Getsemani.

 2. Yesu anapigwa mijeredi.

 3. Yesu anavikwa taji la miiba na anahukumiwa kifo bila hatia.

 4. Yesu anapanda Calvari akibeba Msalaba.

 5. YESU AFA MSALABANI.MAFUMBO YA UKIMYA WA MUNGU

UKIMYA UNAOFANYA KAZI YA MAPENDO NA YA HURUMA

( kwa Jumamosi) :

 1. KRISTO, kati ya siku ya kufa na siku ya kufufuka kwake, siku ya “ukimya wa kimungu” aziweka huru roho za wenye haki na kuwaandalia nafasi mbinguni wao pamoja na wenye haki wengine watakao fuata.

 2. MARIA, kwa Upendo ya Kimama na Mama wa Kanisa zima, kwa licha ya Uchungu wa Kalvari, licha ya “upanga” uliompenya Moyo wake pale Kalvari anapata faraja, anatiwa moyo na kukaa siyo tu na Yohana bali hata Pietro na Mitume wengine wakiwa na uchungu, kuchanganyikiwa na usumbufu wa “kashfa” ya Msalaba.

 3. Huruma ya BABA kwa wanadamu haikatizwi na dhambi ya kumwaga damu na kumwua Mwanae-masiha Yesu Kristo, bali anaipokea kama sadaka jumla ya ukombozi wa wanadamu ambao Mungu aliwapenda, akawaumba kwa sura na mfano wake na kwa ajili ya wokovu wao akamtuma Mwanae wa pekee.

 4. MBEGU iliyoanguka chini kwenye udongo ikafa, maisha ya Kristo yaliyo tolewa sadaka na damu yake iliyo mwagika Kalvari vinachipusha leo hii toka katika ukimya wa kimungu maisha mapya na yasiyaharibika kwa wale wanaoupokea kulingana na mapenzi ya moyo wa Kristo.

 5. ROHO MTAKATIFU, katika kimya kikuu cha Jumamosi anaiandaa na kuifinyanga mioyo na akili za wampendao Mungu ili kulipokea tangazo la Ufufuko lisiloweza kuaminika kibinadamu kwa wale wampendao Mungu, kulipokea lisiloaminika (kibinadamu). Kwa tangazo la ufufuko, maana yeye, Yesu Kristo, “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu: vyote vilifanyika kwa huyo, wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu…Yeye ni Mwanzo na Mwisho, mwezayote …Yeye ni Mwana kondoo asiye na hatia milele yote yuko juu ya altare ya mbinguni na yeye tu mwenye kustahili kuchukua kitabu, kuvunja mihuri yake na kukifungua na kumkabidhi Baba kwa utukufu wa milele wa Mungu, wa malaika zake na watakatifu wake”.

 

MAFUMBO YA UTUKUFU / The Glorious Mysteries

( kwa Jumapili) :

 1. YESU ANAFUFUKA.

 2. YESU ANAPAA MBINGUNI.

 3. ROHO MTAKATIFU ANAWASHUKIA MITUME WAKIWA PAMOJA NA BIKIRA MARIA.

 4. Bikira Maria APALIZWA mbinguni.

 5. Bikira Maria AVIKWA TAJI Mbinguni Malkia wa Mbingu na Nchi.

 

SALAM, MALKIA! / Hail, Holy Queen / Salve Regina

Salam, Malkia! Mama mwenye huruma uzima tulizo matumaini yetu. Salam! Tunakusihi ugenini sisi wana wa Eva. Tunakulilia tukilalamika na kuhuzunika huku bondeni kwenye machozi. Haya basi mwombezi wetu utuangalie kwa macho yako ya huruma, Na mwisho wa ugeni huu utuonyeshe Yesu mzao mbarikiwa wa tumbo lako. Ee mpole, Ee mwema, Ee mpendelevu Bikira Maria.

LITANIA LAURETANA / Litany of Loretto

Bwana utuhurumie!  Bwana utuhurumie!

Kristo utuhurumie!  Kristo utuhurumie!

Bwana utuhurumie!  Bwana utuhurumie!

Kristo utusikie!  Kristo utusikie!

Kristo utusikilize!  Kristo utusikilize!

Baba wa mbinguni, Mungu, Utuhurumie!

Mwana mkombozi wa dunia, Mungu,  Utuhurumie!

Roho Mtakatifu, Mungu,  Utuhurumie!

Utatu Mtakatifu, Mungu,  Utuhurumie!

Maria Mtakatifu,  Utuombee.

Mzazi Mtakatifu wa Mungu,  Utuombee.

Bikira wa Mabikira,  Utuombee.

Mama wa Kristo,  Utuombee.

Mama wa Neema ya Mungu,   Utuombee.

Mama mtakatifu sana,  Utuombee.

Mama mwenye usafi wa moyo,  Utuombee.

Bikira daima,  Utuombee.

Mama usiye na doa,  Utuombee.

Mama mpendelevu,  Utuombee.

Mama mwenye kutamaniwa,  Utuombee.

Mama wa sahuri jema,  Utuombee.

Mama mfariji,  Utuombee.

Mama wa Muumba,  Utuombee.

Mama wa Mkombozi,  Utuombee.

Mama wa Kanisa,  Utuombee.

Bikira mwenye busara,  Utuombee.

Bikira uliyejaa hekima,  Utuombee.

Bikira unayestahili heshima,  Utuombee.

Bikira mwenye nguvu,  Utuombee.

Bikira mwenye huruma,  Utuombee.

Bikira mwaminifu,  Utuombee.

Kioo cha utakatifu wa Mungu,  Utuombee.

Kikao cha hekima,  Utuombee.

Chemichemi ya furaha yetu,  Utuombee.

Tabernakulo ya Roho Mtakatifu,  Utuombee.

Tabernakulo inayong'ara,  Utuombee.

Tabernakulo iliyowekwa wakfu kwa Mungu,  Utuombee.

Tabernakulo ya Aliye Juu,  Utuombee.

Waridi lenye fumbo,  Utuombee.

Binti mteule wa Sion,  Utuombee.

Mnara wa Daudi,  Utuombee.

Mnara wa pembe,  Utuombee.

Mnara imara,  Utuombee.

Hekalu la dhahabu,  Utuombee.

Sanduku la agano,  Utuombee.

Mlango wa Mbinguni,  Utuombee.

Nyota ya asubuhi,  Utuombee.

Afya ya wagonjwa,  Utuombee.

Kimbilio la wakosefu,  Utuombee.

Mfariji wa wenye uchungu,  Utuombee.

Msaada wa Wakristo,  Utuombee.

Malkia wa Malaika,  Utuombee.

Malkia wa Mababu,  Utuombee.

Malkia wa Manabii,  Utuombee.

Malkia wa Mitume,  Utuombee.

Malkia wa Mashahidi,  Utuombee.

Malkia wa Waungama Imani,  Utuombee.

Malkia wa Mabikira,  Utuombee.

Malkia wa Watakatifu wote,  Utuombee.

Malkia uliyetungwa mimba pasipo dhambi ya asili, Utuombee.

Malkia uliyepalizwa Mbinguni,  Utuombee.

Malkia wa Rozari Takatifu,  Utuombee.

Malkia wa familia,  Utuombee.

Malkia wa Amani,  Utuombee.

Mama na Malkia wa Karmelo,  Utuombee.

* Mwana kondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia, utusamee, Bwana.

* Mwana kondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia, utusikilize, Bwana.

* Mwana kondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia, utuhurumie, Bwana.

Utuombee Mzazi Mtakatifu wa Mungu, ili tuweze kustahili ahadi za Kristo.

Tunakuomba, Ee Bwana, utie Neema yako mioyoni mwetu ili sisi tuliojua kwa maelezo ya Malaika kwamba Mwanao Yesu Kristo aliyejifanya mtu, kwa Mateso na Msalaba wake, utuwezeshe kuufikia Utukufu wa Ufufuko. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina.

Ishara ya Msalaba: Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.


Imani Ya Nike / The Nicene Creed
  Ninamwamini Mungu mumoja, Baba Mwenyezi,
Muumba wa mbingu na dunia, 
na vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana.
 
Ninamwamini Bwana mumoja, Yesu Kristo,
Mwana wa pekee wa Mungu,
amezaliwa na Baba mbele ya kuwa ulimwengu, 
Mungu kutoka Mungu, Nuru kwa Nuru,
Mungu kweli kwa Mungu kweli,
amezaliwa, hakuumbwa,
Mwenye umungu mumoja na Baba.
Vitu vyote viliumbwa naye.
Alishuka toka mbinguni,
kwa ajili ya sisi watu,
na kwa ajili ya wokovu wetu;
alitwaa mwili kwa tendo la Roho Mutakatifu,
katika Bikira Maria,
akawa mutu.
Akasulibiwa kwa ajili yetu,
wakati wa Pontio Pilato,
akateswa, akazikwa,
Akafufuka kisha siku tatu,
kama ilivyoandikwa;
akapanda mbinguni,
anakaa kwa mukono wa kuume kwa Baba.
Ndipo atarudi kwa utukufu,
kuwahukumu wazima na wafu,
na ufalme wake hautakuwa na mwisho.
 
Ninamwamini Roho Mutakatifu,
Bwana na Mutoa uzima, 
aliyetoka kwa Baba na Mwana,
anayeabudiwa na kutukuzwa,
pamoja na Baba na Mwana,
aliyesema kwa manabii.
 
Ninaamini Kanisa, moja, takatifu, katolika,
lililotoka kwa Mitume.
Ninasadikia ubatizo mumoja
kwa kuondolewa kwa zambi. 
Ninangojea ufufuko wa wafu

na uzima wa milele utakaokuja.  Amina.

Imani ya Athanasio / The Athanasian Creed

Killa atakae kuokoka: zaidi ya yote imemlazimu kuishika Imani Katholiko. 

Nayo asipoilinda pasipo kuipunguza wala kuiharibu: bila shaka atapotea milele.

Na Imani Katholiko ni hii: tumwabudu Mungu minoja katika Utatu, na Utatu katika Umoja;

Tusizichanganye nafsi: wala kuigawanya asili.

Kwa maana nafsi ya Baba mbali, nafsi ya Mwana mbali: nafsi ya Koho Mtakatifu mbali.

Bali Uungu wa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu ni Uungu umoja: Uttikufu wao sawa, Ukuu wao wa milele.

Kama alivyo Baba, ndivyo alivyo Mwana: ndivyo alivyo Roho Mtakatifu.

Baba hakuumbwa, Mwana hakuumbwa: Roho Mtakatifu hakuumbwa.

Baba hana mpaka, Mwana hana mpaka: Roho Mtakatifu hana mpaka.

Baba wa milele, Mwana wa milele: Roho Mtakatifu wa niilele.

Walakini hakuna watatu walio wa milele: illa Mmoja aliye wa milele.

Kadhalika hakuna wata'tu wasioumbwa, wala watatu wasio na mpaka: illa mmoja tu asiyeumbwa, na mmoja tu asiye na mpaka.

Kadhalika Babani Mwenyiezi, Mwana ni Mwenyiezi: na Roho Mtakatifu ni Mwenyiezi.

Bali hakuna Watatu walio Wenyiezi: illa aliye Mwenyiezi ni mmoja tu.

Yivyo hivyo Baba ni Mungu, na Mwana ni Mungu: na Roho Mtakatif u ni Mungu.

Bali hakuna Miunguwatatu: illa Mungu mmoja tu.

Vivyo bivyo Baba ni Bwana, na Mwana ni Bwana: na Roho Mtakatifu ni Bwana.

Bali hakima Bwanawatatu: illa Bwana mmoja tu.

Kwa maana kama tunavyoshurutishwa kwa kanuni ya kweli ya Kikristo: kukiri ya kuwa killa nafsi ni Mungu na Bwana;

Kadbalika tunagombezwa na Imani Katholiko: tusiseme ya kuwa wako Miungu watatu au Bwana watatu.

Baba hakuumbwa na aliye yote: wala hakukhulukiwa wala hakuzaliwa.

Mwana anatoka katika Baba tu: bakuumbwa, wala hakukhulukiwa, bali anazaliwa.

Roho Mtakatifu anatoka katika Baba na katika Mwana: hakuumbwa,wala hakukhulukiwa, wala hakuzaliwa, bali anatoka.

Bassi yupo Baba mmoja tu, si Baba watatu; yupo Mwana mmoja tu, si Wana watatu: yupo Roho Mtakatifu mmoja tu, si Roho Watakatifu watatu.

Na katika Utatu huu hapana aliye wa kwanza na aliye wa baadae: hapana aliye mkuu zaidi na aliye mdogo.

Bali nafsi zote tatu ni wa milele: wa sawa wote.

Bassi katika mambo yote kama tulivyokwisha kusema: imetulazimu kuuabudu Umoja katika Utatu, na Utatu katika Umoja.

Bassi yeye atakae kuokoka: audhanie hivi Utatu.

Na zaidi ya haya, apate wokofu: imemlazimu kukuamini kwa moyo Kufanyika mwili kwake Bwana wetu Yesu Kristo.

Na Imani kamili ndiyo hii: tuamini, tukiri ya kuwa Bwaiia wetu Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, ni Mungu na Mwana Adamu.

Ni Mungu, ana asili ya Baba, amezaliwa kabla ya zamani zote: ni Mwana Adamu, ana asili ya Mama wake, alizaliwa katika zamani.

Mungu kamili na Mwana Adamu kamili: ana roho yenye akili na mwili wa Mwana Adamu.

Yu sawa na Baba kwa kuwa ni Mungu: Yu chini ya Baba kwa kuwa ni Mwana Adamu.

Na ijapokuwa yu Mungu na Mwana Adamu: yeye si wawili illa Kristo mmoja.

Yeye ni mmoja, si kana kwamba Uungu urnebadilika uwe mwili: bali kwa kuitwaa asili ya Mwana Adamu na kuiunga na Uungu.

Mmoja kabisa; si kwa kuzichanganya asili zile mbili: bali kwa kuwa Nafsi mmoja tu.

Kwa maana karaa roho yenye akili pamoja na mwili huwa Mwana Adamu mmoja: kadhalika Mungu na Mwana Adamu pamoja ni Kristo mmoja;

Aliyeteswa kwa wokofu wetu: akashuka mahali pa wafu, akafufuka siku ya tatu.

Akapaa mbinguni, anaketi mkono wa kuume wa Mungu Baba Mwenyiezi: kutoka huko atakuja kuwahukumu watu wahayi na wafu.

Atakapokuja yeye, wana Adamu wote watafufuka na miili yao: watatoa khabari za matendo yao.

Nao waliotenda mema wataingia katika uzima wa milele: nao waliotenda mabaya katika moto wa milele.

Hii ndiyo Imani Katholiko: killa mtu asiyeikubali kwa moyo hawezi kuokoka.

Utukufu una Baba, na Mwana: na Koho Mtakatifu;

Ulivyokuwa mwanzo: ulivyo sasa, utakavyokuwa milele. Amin.


Usiku mtakatifu! / Silent Night / Stille Nacht
Usiku mtakatifu!
Wengine walala
wakeshao ni Yosefu tu
na Maria, walomlinda
Yesu mwana mzuri
alalaye raha.

"God is Love" in Kiswahili is " Mungu ni Upendo. "

Creative Commons License
The contents of this webpage are licensed under a Creative Commons Attribution 3.0 License.
Valid HTML 4.01 Transitional
(this is the bottom of page)